HTML Tables
Michezo

YANGA WAPEWA ONYO WAAMBIWA KIPIGO KIKO PALE PALE.

Kocha wa Stand United, Athuman Bilal ‘Bilo’, baada ya kuwatambia Simba kwenye mchezo ambao walilazimisha sare ya mabao 3-3, leo amewaambia Yanga wajiandae kupoteza.

Bilo amesema wao ni sawa na Township Rollers ambayo iliifunga Yanga hapa nyumbani kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hivyo wamekuja na tahadhari ya kuchukua alama tatu.

Akizungumza, Bilo ameeleza kuwa wamejiandaa vya kutosha kuelekea mchezo wa leo, huku akisema wanaijua Yanga ambayo ni ya kawaida wala haina makali yoyote.

“Sisi ni kama Township Rollers, tumejiandaa vya kutosha na wala hatuoni ukali wowote kutoka Yanga, tutapambana zaidi kubeba alama tatu leo” amesema Bilo.

Aidha Kocha huyo amewaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi ili kutoa hamasa kwa Stand United ‘Chama la Wana’ kutoa hamasa kwa wachezaji wa timu hiyo.

Click to comment

You must be logged in to post a comment Login

Leave a Reply

To Top