HTML Tables
Michezo

YANGA SC YAONDOLEWA LIGI YA MABINGWA AFRIKA, YAHAMIA KOMBE LA SHIRIKISHO

Yanga imeondolewa rasmi kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika kufuatia suluhu ya 0-0 dhidi ya Township Rollers jioni hii.

Township Rollers wamefanikiwa kusonga mbele mpaka hatua ya makundi, baada ya mchezo wa kwanza uliochezwa jijini Dar es Salaam, kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Kazi nzuri waliyoifanya Township kwenye mechi ya awali, inawafanya Yanga kuyaaga rasmi mashindano hayo na kuwafanya waangukie Kombe la Shirikisho Afrika ambalo Simba anashiriki.

Baadaye Simba SC nayo itakuwa ina kibarua kuanzia majira ya saa  2 na nusu usiku, kukipiga dhidi ya Al Masry huko mjini Port Said, Misri.

Click to comment

You must be logged in to post a comment Login

Leave a Reply

To Top