HTML Tables
Michezo

YANGA SC NA IHEFU ILIKUWA SI KITOTO

KIPA Mcameroon, Youthe Rostand leo ameibuka shujaa wa Yanga baada ya kupangua penalti tatu na kuiwezesha kuingia hatua ya 16 Bora ya michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) kwa ushindi wa penalti 4-3 baada ya sare ya 1-1 ndani ya dakika 90.
Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, Ihefu ya Ligi Daraja la Pili Tanzania Bara ilikaribia kuimaliza Yanga ndani ya dakika 90, kama si bao la penalti la dakika ya mwisho la mshambuliaji Mzambia, Obrey Chirwa.
Ihefu walitangulia kwa bao la kujifunga la beki wa Yanga,
Andrew Vincent ‘Dante’ dakika ya 36 katika juhudi za kuokoa shuti la Innocent Kapalata aliyepasiwa na Elias Salingo.
Baada ya bao hilo, Yanga waliokuwa wakicheza taratibu walikuwa kama waliopigwa mshituko na kuamka kwa kuongeza kasi ya mashambulizi.

Lakini safu ya ulinzi ya Ihefu ikiongozwa na kipa wake hodari, Andrew Kayuni iliwazuia watoto wa kocha Mzambia, George Lwandamina kupata bao.
Kipindi cha pili, Ihefu wakaamua kabisa kucheza kwa kujihami na huku wakipoteza muda kwa kujiangusha na kuchelewa kuanzisha mipira inapofuka upande wao.
Lakini Yanga waliendelea kuwa wastahmilifu huku pia wakibadili mbinu moja baada ya nyingine katika jitihada za kusaka bao la kusawazisha.
Hatimaye mpango wa
kutafuta penalti wa Chirwa ukafanikiwa dakika ya kwanza ya muda wa nyongeza kati ya sita baada ya kutimia dakika 90 za kawaida za mchezo, pale Mzambia huyo alipoingia kwenye boksi na kwenda chini kwa urahisi baada ya kubanwa na mabeki wawili wa Ihefu.
Chirwa mwenyewe akaenda kufunga penalti hiyo na kuwainua kwa furaha mamia ya mashabiki wa Yanga waliokuwa wamenyong’onyea kwa pamoja na baridi ya Mbeya, lakini pia matokeo ya kuwa nyuma kwenye mchezo.
Ukawadia muda wa matuta na kipa wa Ihefu Andrew Kayuni akawashitua Yanga baada ya kuokoa penalti ya kwanza ya Mkongo, Papy Kabamba Tshishimbi – lakini Nahodha Kevin Yondan akarejea kufunga ya pili, Hassan Kessy akafunga ya tatu, Gardiel Michael ya nne kabla ya Chirwa kughongesha mwanmba penalti ya tano na Raphael Daudi kufunga ya sita.
Rostande alicheza penalti za Abubakar Kidungwe, Emmanuel Mamba na Richard Ngondya wakati za Andrew Kayuni, Mando Mkumbwa na Jonathan Mwaibindi zilimpita na kutinga nyavuni.

Click to comment

You must be logged in to post a comment Login

Leave a Reply

To Top