HTML Tables
Michezo

WACHEZAJI HAWA WA YANGA SC KUIKOSA MBAO FC

YANGA SC itaondoka kesho jioni kwa ndege ya Fast Jet kwenda Mwanza tayari kwa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya wenyeji Mbao FC Jumapili Uwanja wa CCM Kirumba mjini humo.
Lakini Yanga itaondoka bila washambuliaji wake wote vinara wa mabao msimu huu, Ibrahim Ajib na Mzambia Obrey Chirwa.
Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa amesema Ajib hatakwenda Mwanza kwa sababu anatumikia adhabu ya kadi tatu za njano wakati Chirwa bado yupo kwao, Zambia kwa matatizo ya kifamilia.
Katika mabao 17 ambayo Yanga imefunga kwenye Ligi Kuu msimu huu, 11 yanatoka kwa wawili hao, Chirwa akiwa amefunga sita na Ajib matano.
Pamoja na wawili hao, Yanga pia itaendelea kuwakosa wachezaji wake majeruhi Wazimbabwe, kiungo Thabani Scara Kamusoko na mshambuliaji Donald Dombo Ngoma pamoja na beki mzalendo, Kevin Patrick Yondan.

Mkwasa amesema Chirwa anatarajiwa kurejea nchini kuanzia kesho na hawezi kujumuishwa kwenye msafara wa Mwanza wazi hatakuwa fiti.
Kwa ujumla Ligi Kuu inatarajiwa kuendelea kesho baada ya mapumziko ya wiki tatu kupisha michuano ya CECAFA Challenge iliyomalizika nchini Kenya wiki iliyopita kwa wenyeji, Harambee Stars kuwa mabingwa wakiwafunga Zanzibar katika fainali.
Kesho Azam FC watakuwa wenyeji wa Stand United Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam kuanzia Saa 1:00 usiku na Jumamosi kutakuwa na mechi tatu, Lipuli na Tanzania Prisons Uwanja wa Samora, Iringa kuanzia Saa 8:00 mchana, Mtibwa Sugar na Maji Maji Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro.

Click to comment

You must be logged in to post a comment Login

Leave a Reply

To Top