HTML Tables
Habari

WAASI DRC WAUA WATU 40

Waasi wa Allied Democratic Forces (ADF) wameuawa watu zaidi ya 40 katika mji wa Beni jimbo la kaskazini la Kivu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

 

Taarifa zinasema, katika hujuma hiyo ya Jumamosi, waasi wa ADF walishambulia kambi kadhaa za kijeshi katika jimbo hilo na kuchukua udhibiti kamili wa kambi tatu.

 

Hali inaripotiwa kuwa tete huku ripoti zikisema waasi hao waliwaachilia huru wafungwa waliokuwa mikononi mwa wanajeshi huku wakiua baadhi ya mateka kiholela.

 

Serikali ya Uganda inawatambua waasi wa ADF kuwa ni kundi la kigaidi. Awali ADF walikuwa na kambi zao magharibi mwa Uganda na sasa wamehamia nchi jirani ya DRC kufuatia oparesheni za jeshi la Uganda.

 

Eneo la Mashariki mwa DRC hukumbwa na machafuko ya mara kwa mara kutokana na kuwepo makundi mengi ya waasi Wakongo na wengine kutoka nchi jirani. Umoja wa Mataifa unasema tokea mwaka 2016 maelfu ya raia wamemuawa katika mapigano mbalimbali katika eneo hilo.

Click to comment

You must be logged in to post a comment Login

Leave a Reply

To Top