HTML Tables
Michezo

VITA INAHAMIA KWENYE KOMBE LA SHIRIKISHO

Kufuatia  kukamilishwa kwa mechi za duru la kwanza la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kalenda ya soka ya Tanzania sasa inahamia kwenye michuano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), ijulikanayo kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) kwa mechi ya hatua ya 32 Bora katikati ya wiki.
Vigogo Azam FC na Yanga SC wote wanasafiri kwenda mikoani kumenyana na timu za Ihefu FC na Shupavu FC katika hatua ya 32 Bora ya michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC).

Yanga SC wanakwenda Mbeya kuifuata Ihefu, mechi itakayopigwa Uwanja wa Sokoine mjini humo, wakati Azam FC watakwenda Uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro kumenyana na Shupavu FC.
Green Warriors iliyowatoa mabingwa watetezi, Simba SC itaendelea kucheza nyumbani mjini Dar es Salaam itakapowakaribisha Singida United Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.

MECHI ZOTE ZA HATUA YA 32 BORA

Maji Maji v Ruvu Shooting
Njombe Mji v Rhino Rangers
Kiluvia Utd v JKT Oljoro
Ndanda Fc v Biashara United
Pamba SC v Stand United
Polisi TZ v Friends Rangers
JKT Tanzania v Polisi Dar
KMC V Toto Africans (Imeahirishwa)
Ihefu FC v Yanga SC
Mwadui FC v Dodoma FC
Green Warriors v Singida United
Tanzania Prisons v Burkina Faso
Kariakoo United v Mbao FC
Maji Maji Rangers Lindi v Mtibwa Sugar
Kagera Sugar v Buseresere FC

Shupavu FC v Azam FC

Click to comment

You must be logged in to post a comment Login

Leave a Reply

To Top