HTML Tables
Habari

UWT PWANI YAHAIDI KUMUUNGA MKONO JPM KWA VITENDO

Jumuiya ya Umoja wa wanawake (UWT) Mkoani Pwani umeahidi kumuunga mkono kwa vitendo  Rais John Magufuli kwa kufanya kazi kwa juhudi na maarifa hali itakayowezesha kuiletea maendeleo Jumuiya hiyo na taifa kwa ujumla.

Hayo yamebainishwa leo na Mwenyekiti wa (UWT) Mkoani Pwani Farida Mgomi wakati wa mkutano wa baraza la umoja huo Wilayani Kibaha likiwa na agenda mbalimbali ikiwemo kuweka mikakati ya utendaji kazi.

“Kauli ya  rais ni kwamba chama kinaiongoza Serikali ili iwatumikie wananchi wote kwa kufuata haki na usawa hivyo sisi viongozi wa jumuiya mbalimbali tunapaswa kuwa mstari wa mbele kufuata mwelekeo huo ili tufike mbali zaidi” amesema

Amesema kuwa katika kulifikia hilo ni vema viongozi wa ngazi mbalimbali wa jumuiya hiyo wakaacha kujiingiza kwenye mgawanyiko wa aina yoyote unaoweza kuwatenganisha na badala yake  wasimamie taratibu na kanuni zinazowaongoza

Kwa upande wake Katibu wa (UWT) Mkoani Pwani Sophia Masawe amesema kuwa njia sahihi itakayowawezesha wanawake  hao kupiga hatua  na kufikia mafanikio ni kudumisha upendo na mshikamano katika utekelezaji wa majukumu yao huku wakiongeza ubunifu wa miradi ya kiuchumi.

Naye Mjumbe wa baraza kuu (UWT) Taifa Nancy Mutaremwa  amesema kuwa  mpango wa jumuiya hiyo kwa sasa ni kujikita katika kubuni na kuanzisha miradi mbalimbali ya kiuchumi ikiwemo ufugaji na kilimo cha mazao ya biashara

1 Comment

1 Comment

  1. Eric Chungu

    Eric Chungu

    January 29, 2018 at 11:52 am

    Ya ahidi. Siyo “yahaidi”

You must be logged in to post a comment Login

Leave a Reply

To Top