HTML Tables
Habari

USHAHIDI WA DAKTARI WA KANUMBA MAHAKAMANI

Mahakama Kuu ya Tanzania imesikiliza ushahidi wa mashahidi wawili akiwemo Daktari wa marehemu Steven Kanumba, Dk.Paplas Kagaiya kwenye kesi ya mauaji ya bila kukusudia inayomkabili Elizabeth Michael ”Lulu’.

 

Mbali ya Daktari huyo, pia ushahidi mwingine umetolewa na Ofisa wa Polisi kutoka Kituo cha Msimbazi, ASP Ester Zefania mbele ya Jaji Sam Rumanyika.

 

Katika ushahidi wake, Dk.Kagaiya akiongozwa na Wakili wa serikali, Batilda Mushi amedai kuwa yeye ni Daktari wa familia ya kina Kanumba.

 

Amesema kuwa anakumbuka April 7, 2012  saa 6 usiku alipigiwa simu na mdogo wa Kanumba ambaye ni Bosco Seth akimwambia Kanumba amedondoka hivyo aende nyumbani akamsaidie.

 

>>>”Nilimwambia Seth kwamba nisingeweza kutoka kwa muda huo kwani sikuwa na usafiri, hivyo nikamwambia kama anaweza anifate,”.

 

Alisema kuwa baada ya muda mfupi, Seth alimfata na gari ambapo alichukua vifaa vyake kisha kuelekea hadi nyumbani kwa marehemu maeneo ya Sinza Vatican.

 

>>>”Tulipofika hatukumkuta mtu yeyeto zaidi ya marehemu ambapo alikuwa amevaa taulo, nilianza kumfanyia vipimo ikiwemo cha sukari na kubaini ni ya kawaidia 4.6, lakini nilipompima B.P nilibaini mapigo ya moyo hayapo kabisa.”

 

Dk.Kagaiya amesema kuwa alibaini kuwa Kanumba ameshafariki ili alihofia kumwambia mdogo wake kwani ingemsababishia matatizo mengine.

 

Dk.Kagaiya amedai kuwa kutokana na hatua hiyo alimwambia Sethi wamvalishe marehemu nguo na wampeleke hospital kubwa ili akafanyiwe vipimo.

 

>>>”Tulimvailisha nguo na kumpeleka hospitaliti ya taifa Muhimbili, ambapo tukafika hadi kitengo cha dharura ambapo alikuja Daktari na kumfanyia vipimo akiwa pale pale kwenye gari na kutuambia Kanumba ameshafariki.”

 

Dk.Kagaiya amesema kuwa baada ya kupewa majibu hayo waliambiwa wafanye utaratibu wa PF.3 wakati mchakato wa kumpeleka Mochwari ukifanyika.

 

>>>”Nilienda kuchukua PF 3 Kituo cha Salenda bridge, ambapo niliongozana na askari watatu hadi kituo cha Oysterbay kwa ajili ya kuandila maelezo.”

 

Alipoulizwa na Wakili Mushi kwamba anamjua Lulu, alijibu anamfahamu kama mpenzi wa Kanumba na siku hiyo ya tukio alionana na Lulu saa 11 alfajiri maeneo ya Sinza Bamaga.

 

>>>”Nilionana na Lulu baada ya kunipigia simu, ambapo baada ya kukutana naye alikamatwa na Polisi,”

 

Alipoulizwa na Wakili wa Lulu, Peter Kibatala kwamba aliwahi kumpima marehemu matatizo ya kichwa, ambapo Dk.Kagaiya alijibu hapana.

 

Pia alijibu kuwa hakujua ni nani aliyemlaza Kanumba chini bali alimkuta yupo chini mwenyewe.

Click to comment

You must be logged in to post a comment Login

Leave a Reply

To Top