HTML Tables
Michezo

UMEWASIKIA MBAO FC! WAIPA ONYO SIMBA SC WASEMA KIPIGO KIKO PALEPALE

Wakati Simba inajiandaa kuendeleza ubabe wake katika Ligi Kuu Bara, wapinzani wao, Mbao FC wanawaza mengine kabisa.
Simba ndiyo vinara wa ligi hiyo na mechi yao ijayo ni dhidi ya Mbao FC kesho Jumatatu. Lakini Mbao licha ya kuwa ugenini, wameapa kuwatuliza vinara hao.

Mbao wamesafiri kutoka Mwanza hadi Dar es Salaam kucheza na Simba mechi hiyo ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa, huku wakiwa na kumbukumbu ya sare ya mabao 2-2 katika mchezo wa awali.
Mwenyekiti wa Mbao, Solly Njashi, ameliambia Championi Jumamosi kuwa, kikosi chao kipo kamili kwa ajili ya kukabiliana na Simba licha ya kwamba wapo ugenini lakini wanataka pointi tatu tu.
“Sisi tupo kamili kabisa kwa ajili ya mchezo wetu na Simba na tumekuja Dar es Salaam kwa ajili ya kusaka pointi tatu, tumekuja kushangaza.

“Kocha Etienne Ndayiragije pamoja na kikosi kizima kimejiandaa madhubuti kabisa kwa ajili ya mchezo huo na tuna imani kwamba tutafanya vyema tena baada ya kutolewa katika Kombe la FA,” alisema Njashi.
Mbao FC wanaamini wao hawashindwi kuwaangusha vigogo kwa kuwa katika mechi ya kwanza ya msimu huu dhidi ya Yanga, Mbao waliifunga Yanga mabao 2-0 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

2 Comments

2 Comments

 1. Issa Ramadhaan Mwinjuma

  Issa Ramadhaan Mwinjuma

  February 25, 2018 at 12:26 pm

  Hiv We Ulie Post Mpira Ni Biasha Kubwa Kama Zilivyo Biashara Zote Je Bila Matangazo Utapataje Wateja? Ssc Hooyeeee Point Tatu Muhimu Kiulainiiii Apo Taifa Home

 2. Paul Kapele

  Paul Kapele

  February 25, 2018 at 12:30 pm

  kila mtu ana haki ya kuongea analoliona

You must be logged in to post a comment Login

Leave a Reply

To Top