HTML Tables
Michezo

UMESIKIA WAZEE YANGA SC BAADA YA KIPIGO MCHEZO WA KIMATAIFA

Ikiwa ni baada ya Yanga kufungwa huku Simba ikiambulia sare katika michuano ya kimataifa, Katibu wa Baraza la Wazee la Yanga, Ibrahim Akilimali amefunguka kuwa ni wazi timu hizo zimejiweka katika mazingira magumu ya kusonga mbele.
Yanga ilifungwa 2-1 na Township Rollers ya Botswana katika Ligi ya Mabingwa Afrika huku Simba ikitoka 2-2 dhidi ya Al Masry ya Misri katika Kombe la Shirikisho, michezo yote ikichezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.
Akilimali alisema timu zetu kimataifa msimu huu hazikuwa na maandalizi, hivyo siyo rahisi kuweza kusonga mbele.
“Ukweli ni kwamba, timu zetu kwenye michuano ya kimataifa msimu huu zimeshindwa, ni vyema wakajipanga kwa ajili ya michuano hii mwakani na siyo kwa sasa.
“Sababu wote wamekutana na timu ambazo zina uwezo na zimejiandaa vyema ndiyo maana zikashindwa kupata matokeo hapa nyumbani na siyo rahisi wao kwenda kupata matokeo huko ugenini ni ngumu sana.
“Wanatakiwa kujipanga upya na kuangalia wapi wamekosea ili kuweza kurudi kwenye mstari lakini kusema watasonga mbele kwenye michuano hii siyo rahisi kabisa,” alisema Akilimali.

Click to comment

You must be logged in to post a comment Login

Leave a Reply

To Top