HTML Tables
Michezo

UMEMSIKIA KOCHA SIMBA SC BAADA YA USHINDI WA JANA

KOCHA Msaidizi wa Simba, Mrundi Masoud Juma amesema kwamba,kutokana na ushindi mnono walioupata dhidi ya Singida United, alitaka kuwadhihirishia wale waliokuwa wanamkashifu juu ya mfumo wake mpya anaoutambulisha kwenye kikosi hicho.

Akizungumza baada ya kumalizika kwa mchezo wao dhidi ya Singida walioibuka na ushindi wa mabao 4-0, Juma alisema, watu walitakiwa kuwa na subira kutokana na kile alichokuwa anafanya lakini badala yake walianza kuongea mengi.
Alisema, mfumo wa 3-5-2 unahitaji wachezaji kujituma zaidi na wanapofika kwenye eneo la 18 kushambulia sana, lakini wachezaji walikuwa hawajazoea kutokana na kilikuwa kitu kipya kwao.

Namshukuru Mungu kwa ushindi wa leo, haikuwa mechi rahisi, Singida ni timu nzuri na kocha wake namuheshimu sana kwa kazi yake, lakini matokeo haya ni kutokana na kutokata tamaa kwani watu waliongea sana juu ya mfumo mpya ndio maana timu ilifanya vibaya Mapinduzi lakini ilitakiwa uvumilivu,” alisema Djuma.
Akizungumzia juu ya ujio wa kocha mpya mkuu wa timu hiyo, Mfaransa, Pierre Lechantre aliyekuja na kocha wa mazoezi ya viungo,
Mmorocco Mohammed Aymen Hbibi, Juma alisema kwanza anamkaribisha sana na anampa maelezo yote juu ya timu tangu alipoikuta na mabadiliko aliyofanya.
Alisema baada ya hapo iwapo ataamua kuendelea na mfumo wa sasa alioanzisha yeye ni sawa na kama ataamua kubadilisha na kuja na falsafa yake yote kwake ni sawa.
“Mimi sina tatizo kabisa, namkaribisha sana, nitampa maelezo yote ya timu tangu nimekabidhiwa na iwapo akiona inafaa kuendelea na mfumo wa sasa au kubadili na kuleta wake yote kwangu ni sawa,” alisema Djuma.
Baada ya matokeo hayo, Simba imeendelea kujichimbia kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Bara wakijikusanyia pointi 29 na michezo 13 waliocheza wakifuatiwa na Azam nafasi ya pili wakiwa na pointi 27, nafasi ya tatu wakiwa Singida United na pointi 23 huku wapinzani wao Yanga wakiwa nafasi ya nne na pointi 22.

Click to comment

You must be logged in to post a comment Login

Leave a Reply

To Top