HTML Tables
Michezo

TETESI ZA USAJILI LEO BARANI ULAYA

Kiungo wa Chelsea N’Golo Kante (26) ni moja ya wachezaji wanaonyatiwa na matajiri wa Ufaransa, PSG. Imeelezwa kuwa matajiri hao wana nia ya dhati ya kutaka kuboresha safu ya kiungo kupitia Kante kwenye msimu wa majira ya joto. Goal.com

Mshambuliaji wa Atletico Madrid, Antoine Griezmann (26) imeripotiwa kuwa tayari ameshaanza kutafuta nyumba mitaa ya Catalan huko Spain kabla ya uhamisho wake kwenda Barcelona haujakamilika. Marca

Juventus ipo katika mipango ya kumsajili kiungo wa Liverpool, Emre Can (24) ifikapo msimu wa majira ya joto. Can atakuwa ameshamaliza mkataba wake mwezi Julai 2018. Liverpool Echo

Kocha wa West ham United, Alan Pardew, amesema atafanya mazungumzo na mmiliki wa timu hiyo ili kuona kama anaweza akasalia kuifundisha ama haitowezekana. Guardian

Click to comment

You must be logged in to post a comment Login

Leave a Reply

To Top