HTML Tables
Habari

TANZANIA YAIBUKA KIDEDEA MAJADILIANO YA MAKINIKIA

Barrick yakubali kulipa Dola Milioni 300 na kuingia Ubia wa 50/50 na Serikali

Waziri Kabudi anasimulia…

Wanabodi  wakati wowote kutoka sasa Taifa litapata mrejesho juu ya taarifa ya mazungumzo kati ya magwiji wa sheria na mambo ya mikataba ya madini na timu ya wataalamu wa Barick, mazungumzo ambayo yamechukua muda Mrefu kutoka na unyeti wake, natumai taifa litabaki kuwa kitu kimoja baada ya Taarifa husika kutufikia na kwamba tutaanza Mwanza mpya wa kuzilinda rasilimali zetu kwa vizazi vijavyo.

 

Heko JPM kwa hatua nzuri uliyotufanya tuifikieMwenyekiti wa Barrick Gold anaongea na kusema Mbele bado kuna matumaini makubwa na wana kazi kubwa ya kufanya na maamuzi yote yanatakiwa yapitishwe na bodi ya wakurugenzi iliyopo Uingereza ambao wanamiliki 64% ya AcaciaMwenyekiti wa Barrick Gold John L. Thornton amesema kulikuwa na kutokukubaliana kati ya Tanzania na kampuni ya Acacia kuhusu masualaya kodi, hata hivyo wamekubali kulipa dola milioni 300 kwa ajili ya kukuza uaminifuKutokana na ugumu wa suala lenyewe wamekubaliana kuunda timu ndogo ambayo itashirikisha pande zote mbili kwa ajili ya kuendelea kushughulikia masuala machache yaliyobakiaMichakato yote itaenda kwa misingi ya uwaziili tuweze kuelewa masuala yote kwa uwazi zaidi .

Napenda kumshukuru rais Magufuli kwa kuwa ndio muanzilishi wa mchakato huu na mfumo huu wa biashara ambao utakuwa ni mfano wa kuigwa duniani, nawashukuru sana….amemaliza Profesa Kabudi anaongea Nawashukuru Rais Magufuli kwa kuchukua hatua za dhati kuhakikisha madini ya watanzania yanawanufaisha wananchi wake,katika kufanikisha hilo uliunda kamati mbalimbali baada ya kujiridhisha kuwa nchi hii rasilimali zake zinaporwa Uliunda Kamati ya Prof. Mruma na kisha baadae kuunda kamati ya Prof. Osoro, haya yalimfanya Prof. Thorton kuja kukuona hapaBaadae uliunda tume nyingine na mimi nikiwa ndio naiongoza , tulianza tarehe 31 Julai na kuihitimisha leo tarehe 19 Oktoba na kutia sahihi tamko la maelewanoMazungumzo haya hayakuwa mepesi hata kidogo, na kuna wakati yalituteteresha sana ila tukafikia makubaliano Mapendekezo ya serikali katika majadiliano yalikuwa haya.

1. kuainisha fidia kutokana na makosa yaliyofanya na kampuni tanzu ya Barrick hapa nchini.

2.Kujadili na kuweka mfumo mpya wa uendeshaji na uchimbaji wa madini ili kuleta mgao sawa kwa makampuni ya madini na serikali

3.Kujadili na kukubaliana muundo na mfumowa uendeshaji utakaowezesha Tanzania kupata manufaa zaidi kutokana na uwekezaji unaofanywa kwenye migodi.

4 Kubadilisha mikataba ya uendeshaji ya migodi MDA’s ili iendane na marekebisho ya sheria ya madini.

 

5 kuhakikisha wananchi wa Tanzania na jamii inayozunguka migodi wanapata faida kutokana na migodi iliyopo katika maeneo yaoBaada ya mazungumzo haya tulikubaliana muelekeo uwe ufuatao

1. Wamekubali masharti yote yaliyopo katika sheria mpya ya madini zilizotungwa na bunge letu na watahakikisha masharti hayo yanaingia kwenye mfumo wa fedha ambao tumekubaliana

 

2.Wamekubali serikali itapata hisa katika migodi hiyo kwa asilimia 16 kama sheria ilivyotamka, lakini pamoja na kumiliki migodi hiyo kwa asilimia 16 kwenye mgao itakuwa nusu kwa nusu

 

3. Migodi hiyo itaweka fedha zinazotokana na madini katika akaunti zilizopo hapa nchini

 

4. Ofisi zao za London na ofisi zao za Johansburg katika siku za usoni zitahamishiwa Tanzania na makao makuu ya kampuni hiyoyawe Mwanza ingawa wanaweza kuwa na ofisi nyingine sehemu nyingine

 

5.Kuanzishakampuni nyingine ya kusimamia na kuendesha migodi na makao makuu yake yatakuwa Mwanza na itaongozwa na mtendaji Mkuu,mkurugenzi wa fedha na mkurigenzi wa manunuzi kutoka Tanzania, na ingawa serikali itakuwa na silimia 16 na mgao wa 50/50 wamekubali serikali itakuwa na wawakilishi katika bodi ya wakurugenzi wa kampuni hiyo katika kila mgodi

 

6. Sehemu kubwa ya kazi zitolewazo mgodini sasa kwa kiasi kikubwa inavyowezekana zitafanywa na kampuni za kitanzania na watanzania

 

7. Kuimarisha huduma za jamii katika maeneo yaliyo karibu na migodi

 

8.Kila kampuni inayoendesha mgodi kuhakikisha inaachana na utaratibu wakutumia wafanyakazi wa mikataba na badala yake kuajiri wafanyakazi wa kudumu ambao ni wazawa na hawatakaa katika makambi ila kwenye makazi na familia zao, na watajenga barabara ili wafanyakazi waweze kutoka kazini na kwenda makwao

 

9.Kuajiri watanzania katika nafasi muhimu na za utaalamu, moja kwa moja au kuwafundisha ili baadae waweze kujaza nafasi za uongozi

 

1O. Kutenga bajeti maalumu kwa ajili ya kuchangia utafiti wa kuendesha utafiti wa kuanzisha kiwanda cha kuchakata makinikia na kujenga maabara kubwa ya kupima makinikia

 

11.Serikali itakuwa na umiliki wa madini yote (rare metals) kama zitapatikana, wao watabaki na dhahabu, shaba na fedha, mafanikio haya sio madogo hata kidogo

 

12. Kesi zote na mashauri yote yatafanyika hapa Tanzania na sio nje kama ilivyokuwa zamani

 

13. Suala la fidia lilikuwa suala gumu sana na ndilo lililochukua muda mrefu lazima tupitie nyaraka, ila wamekubali kutoa dola milioni 300 wakati mazungumzo ya jambo hilo yanaendela.

Watanzania tuna kila sababu ya kumshukuru Rais Magufuli kwa azma ya kusimamia mambo haya kidete na kwa nguvu zote na kututia moyo na kutuamini sisi badala ya kuleta wataalamu kutoka nje.

 

50/50 Barrick waliyokubali ni hatua kubwa na mazungumzo yaliyosalia tutafikia muafakaProf. Kabudi amemaliza kuzungumza, sasa anazungumza Rais Magufuli

1 Comment

1 Comment

  1. Nixon Jasson

    Nixon Jasson

    October 19, 2017 at 4:49 pm

    Nadhani ni wakati muafaka sasa kwa wakubwa wetu kuwalipa wale WADENI kule NJE ili kujenga taswira njema ya nchi yetu. Maana kiasi hiki cha takriban sh 660bn sio haba hata kidogo. Naiona ndege yetu ‘ikiwasili’ hapa nchini hivi karibuni.

You must be logged in to post a comment Login

Leave a Reply

To Top