HTML Tables
Habari

TANZANIA NA OMAN KUANZISHA SOKO LA PAMOJA KUKUZA UTALII

TANZANIA NA OMAN ZAFANYA MAZUNGUMZO YA KUANZISHA SOKO LA PAMOJA LA KUKUZA SEKTA YA UTALII

 

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt.Hamisi Kigwangalla amesema Tanzania na Oman zimefanya mazungumzo ya pamoja ya namna ya kukuza sekta ya Utalii baina ya nchi hizo mbili ambapo zitashirikiana katika muingiliano wa Watalii watakaokuwa wakitokea moja kwa moja Oman na kuja Tanzania.

 

“Tumeweza kuzungumzia ushirikiano wa sekta ya Utalii. Hii ni pamoja na kuanzisha soko la pamoja kati ya Oman na Tanzania. Watalii wanaokwenda Oman wanaotaka kuja nchi za Afrika basi waunganishwe moja kwa moja kutoka Oman na kuja Tanzania kwani wenzetu wana watalii wengi kuliko sisi. Hivyo ujio wao hapa nchini ni faida kubwa kabisa na tumejifunza mengi katika sekta hii

 

“Pia tumeweza kujifunza namna wenzetu wanavyoitangaza nchi yao  na sisi tutatumia uzoefu huo kuboresha sekta hii ya Utalii kama dhamana tuliyopewa” alieleza Dk. Kigwangalla.

Awali Dk. Kigwangalla aliweza kutembelea meli hiyo ya kifahari ya Mfalme wa Oman Mhe. Qaboos bin Said ‘Fulk Al Salamah’ iliyofika mapema juzi Jijini Dar e Salaam ikiwa katika msafara wa kitaifa kati ya Serikali ya Oman na Tanzania.

 

Katika tukio hilo Mhe. Kigwangalla aliungana na msafara wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan katika chakula cha mchana ndani ya Meli hiyo ya Mfalme wa Oman Mhe. Qaboos bin Said ijulinakanyo kama ‘Fulk Al Salamah’.

 

Meli hiyo ya kifahari ya Mfalme wa Oman ipo nchini hadi Oktoba 21.2017 kwa ajili ya kusambaza ujumbe wa ‘Amani na Upendo’ duniani, ambapo  baadaye itaelekea Mombasa nchini Kenya kwa madhumuni hayo hayo.

Click to comment

You must be logged in to post a comment Login

Leave a Reply

To Top