HTML Tables
Michezo

SPORTPESA YAWAKABIDHI VIFAA VYA MICHEZO WABUNGE

Kampuni ya kubashiri Tanzania SportPesa imewakabidi vifaa vya michezo wabunge wa Bunge la Tanzania kwa ajili ya michuano ya mashindano ya wabunge wa Afrika Mashariki inatakayoanza kesho katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam


Akikabidhi vifaa hivyo Mkurugenzi wa Utawala na uendeshaji wa SportPesa Tarimba Abas amesema kwamba wametoa vifaa hivyo kwa wabunge ili viweze kuwapa molari kwenye michuano hiyo kikubwa hapa Afrika Mashariki.

“Nia yetu ni kuwasaidia wabunge wetu ili wawe na molari ya kucheza na kuhakikisha wanaibuka mabingwa wa michuano hiyo,maana vifaa tulivyotoa vimejumuisha michezo yote watakayoshiriki kuanzia kesho.

“Utaona tumetoa jezi za mpira wa miguu,mpira wa Pete mpira wa wavu na mingine mingi,” alisema Tarimba.
Kampuni hiyo ya michezo ya kubashiri nchini, imejitolea kwa kiasi kikubwa kusaidia michezo na hasa soka kwa hapa nchini.
Kwa sasa ndiyo kampuni inayodhamini zaidi michezo kuliko nyingine zote.

Click to comment

You must be logged in to post a comment Login

Leave a Reply

To Top