HTML Tables
Habari

SOMALIA INAOMBOLEZA VIFO VYA RAIA 276

Idadi ya vifo kutokana na shambulizi la bomu kwenye makutano ya KM5 karibu na hoteli moja maarufu mjini Mogadishu, Somalia sasa vimedhibitishwa kufika 276 huku watu wengine wapatao 300 wakisemekana kujeruhiwa, waziri wa habari wa Somalia Abdirahman Osman amesema.  

 

Mlipuko huo ambao umetajwa kama shambulizi mbaya zaidi katika historia ya Somalia ulitokea Jumamosi alasiri wakati lori lililokuwa na bomu lilipolipuka mbele ya hoteli ya Safari .

“Kwa miaka kumi ambayo nimefanya kazi hapa Somalia sijawahi kuona maafa kama haya,” daktari mmoja wa shirika la kutoa huduma za ambulensi ya Aamin aliambia kituo cha VOA.

 

Wakati huo huo hospitali mjini Mogadishu sasa zimetoa maombi ya damu ili kuokoa mamia ya watu waliojeruhiwa kwenye mlipuko huo.   Waziri Osman, kupitia kwa ujumbe wa Tweeter, amelaumu kundi la kigaidi la Al Shabaab kwa mauaji hayo.

 

Hata hivyo kundi hilo halijajitokeza na kukiri kuhusika katika shambulizi hilo la Jumamosi. Shambulizi hilo limekemewa vikali na jamii ya kimataifa.

Click to comment

You must be logged in to post a comment Login

Leave a Reply

To Top