HTML Tables
Michezo

SIMBA SC IKIWA KAMILI IMETUA MORO

TIMU ya Simba SC imewasili mjini Morogoro kuweka kambi ya kujiandaa na mchezo wake ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Singida United Januari 18, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Simba SC imeweka kambi katika Chuo cha Biblia, Bigwa mjini Morogoro na leo jioni inaanza mazoezi kujiandaa na mchezo huo unaotarajiwa kuwa wa ushindani mkali kutokana na timu zote kuwa kwenye mbio za ubingwa.
Mshambuliaji Mganda, Emmanuel Okwi aliyekuwa kwao kwa sababu ya mapumziko maalum aliyopewa kupata ahueni ya mapumziko maalum aliyopewa kupata ahueni ya maumivu yake amepona na amerejea – naye pia yuko kambini mjini Morogoro.

 
Kipa namba moja, Aishi Salum Manula aliyepewa ruhusa ya kwenda kuoa, kipa namba mbili Said Mohammed Nduda aliyekuwa majeruhi wote wapo kambini Morogoro.

Na baada ya timu kufanya vibaya kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar, viongozi wanatarajiwa kukutana na wachezaji kuwarudishia morali iliyopotea kabla ya mchezo na Singida.

Ndani ya Simba inaaminika hakuna tatizo isipokuwa tu morali iliyopotea kutokana na mambo ambayo yanasuluhika na kuelekea kwenye Ligi Kuu, matarajio bado ni ubingwa kwa Wekundu wa Msimbazi.
Simba SC inaongoza Ligi Kuu kwa pointi zake 26, sawa na Azam FC, wakiizidi kwa pointi tatu Singida United na tano mabingwa watetezi, Yanga SC.
Ligi Kuu inarejea leo baada ya mapumziko ya wiki mbili kupisha michuano ya kombe la Mapinduzi, inayofikia tamati leo usiku visiwani Zanzibar kwa mchezo wa fainali kati ya Azam FC na URA ya Uganda.

Click to comment

You must be logged in to post a comment Login

Leave a Reply

To Top