HTML Tables
Burudani

SHILOLE APATA MWANAUME MPYA

Na Thomas Samson

Staa wa bongo movi pamoja na bongo fleva mwanadada Zuwena Mohamed maarufu kama “shilole” au “shishi baby” amejinadi kupata mwanaume ambaye yupo tayari kifunga nae pingu za maisha.

Vyanzo mbalimbali vya karibu na staa huyo vimedai amepata mwanaume dereva bodaboda na mahusiano yao ni ya siri hata ndoa yao pia itakuwa ya siri kutokana na hali ya uchumi ya mwanaume huyo

“Ni kweli nina mchumba lakini sio dereva bodaboda ni fundi magari,tuko kwenye mipango ya ndoa na harusi yetu haitakuwa ya siri itakuwa wazi na tutafunga kwenye ndege” alizungumza  shilole akikanusha madai ya kuwa na dereva bodaboda na kujinadi kuwa na mipango ya kufunga ndoa kwenye ndege

Click to comment

You must be logged in to post a comment Login

Leave a Reply

To Top