HTML Tables
Habari

SERIKALI YASEMA IKO TAYARI KUMTIBU TUNDU LISSU

Serikali imesema ipo tayari kugharamia matibabu zaidi ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu popote duniani.

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ameeleza hayo leo Alhamis kuwa watafanya hivyo pindi watakapopata maombi kutoka kwa familia pamoja na taarifa kutoka kwa madaktari kuhusu mahitaji ya matibabu zaidi ya mgonjwa.

Taarifa hiyo ya Ummy imekuja muda mfupi baada ya Mbunge wa  Singida Kaskazini(CCM), Lazaro  Nyalanduakusema kwamba madaktari wa Kenya wamesema Lissu  hawezi kusafirishwa kwenda nje kwa ajili ya kumpatiwa matibabu.

Mbunge Nyalandu ameeleza hayo kwenye ukurasa wake wa Instagram, Facebook na Twitter  kwamba  mipango ya kumsafirisha  Lissu ambayo walikuwa wanafanya itasimama kwa sasa  kutokana na ushauri wa madaktari hao  ili kuruhusu kukamilishiwa huduma za tiba ambazo tayari ameanzishiwa, hadi hapo itakavyoshauriwa vinginevyo

12 Comments

12 Comments

 1. Nixon Jasson

  Nixon Jasson

  September 21, 2017 at 1:48 pm

  Tatizo ni moja tu kwamba wao hung’ang’ani kuwatibu viongozi kule kwenye hospitali ‘yao’ ya Apollo nchini India!!!

 2. Pingback: Tracy Mckay

 3. Pingback: Ivon Gregory

 4. Pingback: creditmattersinc.org

 5. Pingback: Odell Sullivan

 6. Pingback: 2019

 7. Pingback: cleantalkorg2.ru

 8. Pingback: #macron #Lassalle

 9. Pingback: a2019-2020

 10. Pingback: facebook

 11. Pingback: facebook1

 12. Pingback: javsearch.mobi

You must be logged in to post a comment Login

Leave a Reply

To Top