HTML Tables
Burudani

SAIDA KAROLI: ORUGAMBO IMENIRUDISHA VIZURI, NGOMA KALI ZINAKUJA

Msanii na mwimbaji wa nyimbo za asili nchini Saida karoli akiri kurudishwa na Orugambo nyimbo ambayo imemfanya asimame mpya kwa mara nyingine tena kutokana na kazi hiyo kupata mapokeo makubwa hasa kwa mashabiki wake.

 

Saida amesema nyimbo ya ‘Orugambo’ imempa nguvu kubwa katika ujio wake huu na anawaahidi mashabiki wake na wapenzi wa muziki wa asili wategemee makubwa zaidi ambayo atayafanya Saida Karoli katika muziki wake.

 

Hata hivyo,ameongeza kuwa atajikita zaidi katika kufanaya ‘Show’ nyingi ndani na nje ya nchi na sio tena kujikita katika Album kama ilivyokua katika soko la muziki hapo zamani kwa kuwa uuzaji wa Album unachangamoto nyingi hususani kwa maharama wa kazi za wasanii ambao wamekuwa wakinufaika zaidi kuliko wasanii.

 

‘’Ninakazi nyingi sana ambazo nimefanya na wasanii wa ‘Bongo Fleva’ na pia wakae mkao wa kula kwani nina nyimbo nzuri sana amabayo nimefanaya na ‘Rayvan’ msanii kutoka ‘WCB’ amesema Saida karoli.

 

Saida kwa sasa anafanya vizuri na yake mpaya inayokenda kwa jina la ‘Kichaka’ nyimbo amabayo amewashirikisha wasanii wa Bongo Fleva G Nako na Belle9.

Click to comment

You must be logged in to post a comment Login

Leave a Reply

To Top