HTML Tables
Burudani

RONEI: NATAMANI SANA KUFANYA KAZI NA VANESSA MDEE

Msanii wa muziki kizazi kipya Ronei ambaye kwa Mara ya Kwanza kabisa amejitambulisha Vyema Baada ya kufanya vizuri kwenye wimbo Wa Nundu alioshirikishwa na Harmorapa Amesema Anatamani Siku Moja kufanya kazi Na Mwanamuziki Vanessa Mdee

Akizungumza katika kipindi cha Yetu Mseto Kinachorushwa na Yetu Radio Ronei Amesema anashukuru kwa namna Wadau walivyoupokea wimbo Huo.

“Unajua Mwanzo sikutarajia kama ntaipata Hii Fursa ilikuwa Ghafra tu napata Taarifa za  kuhitajika studio Kuimba kiitikio katika wimbo huu , lakini Namshukuru Mungu niliitikia wito na nikafanya kitu ambacho hata Wadau wanaonekana kukikubali” Alisema Ronei.

Msanii Huyo Amesema Kwake Huo ni Mwanzo Mzuri Ambapo kupitia Sabuka Music na Meneja wake P.Funk Majani,  anaamini Kuna kazi Nzuri Zaidi zinakuja

Kwa upande Mwingine Ronei Amedai anavutiwa sana Na Uimbaji wa Mwanadada Vanessa Mdee Huku akitamani kufanya kazi na Msanii Huyo Siku Moja.

“Kiukweli nampenda sana Vanessa Mdee na Staili yake Ya uimbaji kwangu ni kivutio kikubwa sana, Lengo langu ni kukutana Na msanii Huyu Ili Tufanye kazi pamoja Namkubali sana Popote alipo Ujumbe Huu Umfikie” Aliongeza Ronei

Click to comment

You must be logged in to post a comment Login

Leave a Reply

To Top