HTML Tables
Burudani

PRIYANKA CHOPRA APATA SHAVU ZAIDI KWENYE QUANTICO SEASON 3

Staa wa Quantico, Priyanka Chopra ameongezewa episodes 13 za tamthilia hiyo katika Season 3

Mrembo huyo wa India ambaye amafanya vizuri nchini Marekani amethibitisha hilo kupitia mtandao wa Twitter kwa kuandika, “So excited about the season 3 pick up for #Quantico congrats to everyone who made it happen! #AlexParrish will be back soon...”

Alhamisi ya mwezi Februari ya mwaka huu Chopra alikimbizwa hospitali baada ya kuumia wakati akiigiza kwenye tamthilia hiyo na kuteleza na kuangukia kichwa.

Quantico ambayo inaendelea kutayarishwa mjini New York, Marekani inaonyeshwa katika kituo cha runinga cha ABC. Kwa mujibu wa Nielsen umetangaza kuwa season 2 ya tamthilia hiyo iliyokuwa na episodes 21 ilifanikiwa kutazamwa na watu milioni 2.8 ikiwa ni idadi ndogo zaidi katika utazamwaji wa tamthilia hiyo.

1 Comment

1 Comment

  1. Rajab Ayoub

    Rajab Ayoub

    May 18, 2017 at 12:54 am

    atari sasa uyu mtuu au mm rjb

You must be logged in to post a comment Login

Leave a Reply

To Top