HTML Tables
Michezo

NYOTA SABA YANGA SC KUIKOSA AZAM FC LEO

MZUNGUKO wa 15 wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara unatarajiwa kuendelea leo kwa mechi nne, lakini kubwa zaidi ni kati ya Azam FC na Yanga SC Uwanja wa Azam Complexm, Chamazi, Dar es Salaam kuanzia Saa 10:00 jioni.
Mechi nyingine za leo Mwadui FC watakuwa wenyeji wa Njombe Mji FC Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga, Mbeya City watakuwa wenyeji wa Mtibwa Sugar Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya na Kagera Sugar wataialika Lipuli FC Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.
Yanga wanaifuata Azam FC kinyonge leo bila wachezaji wake saba ambao ni mabeki Pato Ngonyani, Abdallah Shaibu ‘Ninja’, viungo Pius Buswita, Thabani Kamusoko na washambuliaji Amissi Tambwe, Yohana Nkomola na Donald Ngoma.

 

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa klabu, Dissnas Ten, wachezaji wote watakosekana kwa sababu ni majeruhi, wakati kiungo Pius Buswita yeye hatakuwepo kwa sababu anatumikia adhabu ya kadi tatu za njano.

Huku pia Yanga ikaendelea kumkosa kocha wake mkuu, Mzambia George Lwandamina ambaye hadi jana jioni alikuwa bado hajapatiwa kibali cha kufanya kazi nchini, ingawa uongozi ulisema ulikuwa unakaribia kupatiwa.

1 Comment

1 Comment

  1. Paul Kapele

    Paul Kapele

    January 27, 2018 at 10:43 am

    kama yanga wamekua wanyonge toka kambi yao mi nadhani wakifika uwanjani watapoteana na kupelekea kipigo.

You must be logged in to post a comment Login

Leave a Reply

To Top