HTML Tables
Michezo

NINJE APEWA TIMU YA TAIFA

Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), limemteua kwa muda, Ammmy Ninje, kuwa Kocha wa muda wa Timu ya taifa ya Vijana wenye chini ya miaka 20, Ngorongoro Heroes.

Ammy Ninje ametangazwa leo na Shirikisho hilo ili kuiandaa Ngorongoro Heroes kwa ajili ya michezo miwili ya kirafiki dhidi ya Morocco na Msumbiji ikiwa ni kabla ya kucheza na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuelekea AFCON U20.

Ngorogoro Heroes itacheza na timu ya Taifa ya Vijana ya Morocco Jumamosi ya Machi 17, 2018 na dhidi ya timu ya Taifa ya Vijana Msumbiji, Jumatanoya Machi 21, 2018. Michezo yote ikichezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali za AFCON U20, Ngorogoro Heroes itacheza dhidi ya DR Congo Machi 31 katika uwanja wa Taifa, na mchezo wa marudiano kufanyika baada ya wiki mbili jijini Kinshansha Congo DR.

Click to comment

You must be logged in to post a comment Login

Leave a Reply

To Top