HTML Tables
Michezo

NEVILLE ASEMA NANI MWENYE NAFASI YA KUWA MCHEZAJI BORA WA DUNIA KATI SALAH NA RONALDO

CRISTIANO Ronaldo ndiye mwenye nafasi kubwa ya kutwa tuzo ya mchezaji bora wa dunia, Ballon d’Or.

Hayo ni maoni ya ‘Mkali’ wa Sky Sports, Gary Neville akikata mzizi wa fitini juu ya uwezo mkubwa unaoonyeshwa na Mmisri Mohamed Salah hadi kufikia wadau wa soka kuanza kumtaja kama mpinzani mkuu wa Ronaldo na Messi kwenye tuzo hiyo.

Ronaldo amekuwa katika kiwango bora sana tangu kuanza kwa mwaka 2018 huku hadi Aprili hii akiwa tayari ameshaifungia Real Madrid mabao 26 kwenye michuano yote.

Nahodha huyo wa Ureno ni kama vile alijifungia na Lionel Messi katika chumba cha Ballon d’Or kwa takribani miaka 10 sasa wakipokezana kutwaa tuzo hiyo bila nyota mwingine yeyote

Licha ya Salah kuonyesha kiwango bora huku akimiminiwa sifa kemkem, bado Neville anaamini huu ni mwaka wa Ronaldo kutwaa tuzo yake ya sita ikiwa ni pamoja na kuisaidia Madrid kuibuka mabingwa wa Ulaya kwa mara ya tatu mfululizo.

Click to comment

You must be logged in to post a comment Login

Leave a Reply

To Top