HTML Tables
Michezo

NANI ALIKUDANGANYA MANARA KAONDOKA SIMBA SC!!

Baada ya kuenea kwa taarifa zilizoeleza kuwa Ofisa wa Habari katika klabu ya Simba. Haji Manara, kuwa anataka kuachia ngazi, Manara ameibuka na kukanusha.

Manara ameeleza hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram hivi punde akisema hawawezi akaondoka Simba wakati mgumu kama huu huku akiwataka Wanasimba kilichotangazwa ni uzushi.

Awali baadhi ya mitandao na vyombo kadhaa vya habari vieleza kuwa yawezekana Manara akawa anataka kuachia ngazi kufuatia kauli ya mafumbo aliyoaiandika jana katika ukurasa wake wa Instagram ambayo ilishindwa kutafsrika kirahisi.

Kushindwa kueleweka kwa kauli hiyo kirahisi, kiliwafanya baadhi ya wadau wa soka na vyombo kadhaa vya habari kuripoti kuwa pengine Manara anaashiria kuachana na vinara hao wa ligi msimu huu.

“Siondoki Simba na naomba muelewe hvyo, ninafanya kazi sehemu sahihi na wakati sahihi. Rafiki zangu na washabiki wa klabu muelewe hvyo. Walichokitangaza ni uzushi, nawezaje kuwaacha Simba kipindi hiki muhimu?” ameandika Manara.

Click to comment

You must be logged in to post a comment Login

Leave a Reply

To Top