HTML Tables
Michezo

MTOTO WA RAIS WEAH HUENDA AKAPOTEZEA NCHI YAKE

Mtoto wa mwanasoka wa zamani na Rais wa sasa wa Liberia George Weah, Timothy Weah huenda asiichezee timu ya taifa ya Liberia kutokana na kuanza kuchezea timu za vijana za taifa la Marekani ambako amezaliwa.

Timothy ambaye  juzi jumamosi amecheza mechi yake ya kwanza ndani ya klabu yake ya PSG ya Ufaransa ambayo hata baba yake aliichezea, aliingia dakika ya 78 akichukua nafasi ya Giovani Lo Celso katika mchezo ambao PSG iliibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Troyes.

Timothy alizaliwa miaka 18 iliyopita jijini New York nchini Marekani, hivyo anatambulika kama raia wa nchi hiyo na tayari ameshaitumikia timu ya Taifa ya vijana ya Marekani katika ngazi tofauti.

Chipukizi huyo anayecheza nafasi ya ushambuliaji kama baba yake huenda asiichezee Liberia kutokana na kanuni za FIFA kuzuia mchezaji kuchezea mataifa mawili lakini endapo tu ataitwa kwenye timu ya taifa ya wakubwa Marekani na kuichezea katika michuano inayotambulika na FIFA.

Click to comment

You must be logged in to post a comment Login

Leave a Reply

To Top