HTML Tables
Michezo

MTIBWA SUGAR YAPOKEA KIPIGO MBEYA.

Kipute cha Ligi Kuu Bara kimeendelea tena leo kwa viwanja kadhaa kutimua vumbi, huku mchezo mmoja (Azam FC vs Mbao FC) ukisubiriwa kuanza majira ya saa moja.

Ruvu Shooting imegoma kupapaswa nyumbani baada ya kwenda sare ya mabao 2-2 dhidi ya Mbeya City FC.

Singida United ikiwa katika Uwanja wake wa nyumbani, Namfua Stadium, imelazimishwa suluhu ya bila kufungana dhidi ya Ndanda FC kutoka Mtwara.

Majimaji FC imezidi kujiweka kwenye mazingira magumu baada ya kupata suluhu ya 0-0 dhidi ya Lipuli FC yenye maskani yake mjini Iringa.

Nayo Mtibwa Sugar iliyosafiri kuelekea mjini Mbeya, imekunali kuchapwa mabao 2-1 dhidi ya Tanzania Prisons, mechi ikipigwa Uwanja wa Sokoine. Mabao ya Prisons yamefungwa na Kimenya katika dakika ya 45 na 49, huku la Mtibwa likifungwa na Mbonde dakika ya 32.

Mechi ya Azam FC dhidi ya Mbao itaanza saa 1 kamili jioni hii kwenye Uwanja wa Azam Complex.

Click to comment

You must be logged in to post a comment Login

Leave a Reply

To Top