HTML Tables
Burudani

MSAMI: NATAKA TUZO ZA ‘BET’ , MUZIKI WANGU NAUELEKA KIMATAIFA

Mwanamuziki wa kizazi kipya Msami amesema anatamani kufikia viwango bora vya kimataifa hadi kuwania tuzo maarufu kama BET kupitia muziki wake na kwamba anapambana kufanya kazi nzuri ili aweze kuyafikia malengo yake.

Msanii wa Kizazi Kipya MSAMI

Msami ameyasema hayo alipokuwa na anazungumza na kipindi cha new tempo beat kinachorushwa na Yetu redio kila siku kuanzia saa nane mchana mpaka saa kumi jioni.

Msami anaetamba na kibao chake kijulikanacho kama WAHENGA amesema amesema kwa sasa ana lengo la kuupeleka muziki wake kimataifa zaidi

“Kwa hapa nyumbani nadhani nafahamika sana ila sasa lengo langu ni kwenda kimataifa zaidi hadi na mimi niweze kushiriki kwenye tuzo kama BET” Alisema Msami

Na alipoulizwa kuhusu video ya wimbo wake mpya, Msami alisema anatarajia kutoa video ya wimbo huo takribani wiki mbili zijazo na aliongeza kuwa video zake anafanyia hapa hapa nchini ili kudumisha uzalendo.

Click to comment

You must be logged in to post a comment Login

Leave a Reply

To Top