HTML Tables
Burudani

MKALI WA WIKI: NYOTA WA WIMBO WA UNIRUDISHIE FURAHA YANGU ,ASEMA ANAMKUBALI SANA GOODLUCK GOZBERT.

Vedastus Mpemba Mwimbaji wa Nyimbo za Injili

MAHOJIANO NA MUIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI VEDASTUS MPEMBA

YETU MEDIA:Habari Vedastus Mpemba Karibu Sana Kwenye Kipengele cha Mkali wa wiki

VEDASTUS: Asante Sana Mkuu Nashukuru

YETU MEDIA: Wiki Hii wimbo wako Wa Unirudishie Furaha yangu Unaonekana kufanya vizuri kwenye Vyombo vya Habari hasa kwenye Vipindi vya Dini Unaweza kutueleza historia yako kwa Ufupi

VEDASTUS: Naitwa Vedastus Mpemba ni mzaliwa wa mkoa  shinyanga mm ni msukuma kwa ufupi nimetokea familia ya kati mama angu ni mwalimu na baba ni daktari, mimi ni mtoto wa mwisho Kati ya watoto wanne Mungu aliowajalia wazazi Wangu maisha yangu  yamekua na changamoto mbalimbali tangu nilipomaliza kidato cha nne nilianza kujishughulisha na shughuli za kujitafutia ili nipate riziki kwani niliona nimeshakuwa mtu mzima katika utafutaji nimepitia vipindi tofauti tofauti huku sehem kubwa ikiwa ni changamoto ya uchumi katika kujiendeleza kimaisha ila namshukuru Mungu kutokana na vipawa alivyonipa niliendelea kufanya juhudi ili kuviendeleza na kujikuta vinanisaidia katika uendeshaji wa maisha mimi ni artist, composer, story writer, actor, designer ,producer nani Mc katika kujishughulisha nimepata mafanikio kiasi nikaanza kujisapoti kuvikuza zaidi vipaji vyangu na hadi kufikia hatua hii niliyofika namshukuru Mungu kwani naamini hapa nilipofika ndoto zangu zote zinakwenda kutimia

YETU MEDIA: Ni Kwanini uliwaza kuuita wimbo wako Nirudishie Furaha

VEDASTUS: Niliwaza hii Idea nirudishie furaha kutokana na changamoto mbalimbali za maisha nilizowahi kupitia na zile nilizoziona kwa ndugu na marafiki nilijikuta naingiwa na huzuni pale unapojikuta unapata tatizo na kupoteza baadhi ya vitu vya muhimu kwako halafu furaha inapotea na kuhisi hakuna mtu anaeweza kuirudisha na hapo ndipo wengi humkumbuka Mungu na kuona ndo msaada pekee katika lile tatzo lililotokea, hapo ndipo nilipata chorus ya nirudishie furaha yangu

YETU MEDIA : Malengo yako ni kufika Wapi Kwenye Muziki wa Injili

VEDASTUS : Malengo yangu kwanza ni kuufanya muziki wangu na muziki wa injili kuendelea Kukua zaidi kimataifa yaani nataka niwe na bendi yangu itakayokua inafanya live pia kuwasaidia vijana wenye vipaji kama mimi hasa wale wasio na uwezo kabisa kiuchumi especially mayatima , na pia nina malengo ya kufungua shule ya muziki ili kuviinua vipaji vya watoto wetu wakitanzania vikue kufikia level ya kimataifa ili kupitia muziki watu wamjue Mungu tunaemwabudu na uamsho wa injili uwe kwa kiwango cha juu

YETU MEDIA: Muimbaji Gani wa Nyimbo za  Injili unamkubali

VEDASTUS : Mwimbaji wa muziki wa injili anaenivutia sana ni Goodluck Gozbert japo wapo wengine wengi tu ninaovutiwa nao ila zaidi ni yeye Kwani pia ni kijana kama mimi na ndie pekee alieonyesha uthubutu mkubwa na hata kuamsha hisia za wengi katika muziki wa injili

YETU MEDIA : Asante Sana Karibu wakati Mwingine…

VEDASTUS : Nashukuru sana

Mwimbaji Goodluck Gozbert, ambaye Vedastus Mpemba Kasema Ndio Amekuwa kivutio kikubwa kwake kutokana na Uimbaji wake

Click to comment

You must be logged in to post a comment Login

Leave a Reply

To Top