HTML Tables
Michezo

MFARANSA WA SIMBA SC AANZA KAZI LEO

Raundi ya kwanza ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inahitimishwa leo kwa michezo miwili, vinara Simba SC wakiwakaribisha Maji Maji ya Songea Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam na Singida United watakuwa wenyeji wa Tanzania Prisons Uwanja wa Namfua mkoani Singida.
Kwa Simba SC mchezo wake wa leo una taswira mbili, kwanza ni kuendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ili kumaliza kileleni baada ya duru la kwanza katika harakati zake za kutwaa ubingwa wa kwanza wa Ligi Kuu baada ya miaka mitano.

Lakini pia ni kuwapa fursa mashabiki wake kujionea soka ya timu hiyo chini ya kocha mpya, Mfaransa Pierre Lechantre anayesaidiwa na Mrundi Masoud Juma, kocha wa viungo Mohamed Aymen Hbibi na kocha wa makipa  mzawa, Muharami Mohammed ‘Shilton’.

Lechantre alianza kazi Jumatano wiki hii Uwanja wa Chuo cha Bandari, Tandika mjini Dar es Salaam baada ya timu kurejea kutoka Bukoba ambako Jumapili iliyopita walishinda 2-0 dhidi ya wenyeji, Kagera Sugar chini ya kocha Masoud Juma.
Na baada ya takriban siku tatu za kuweka ujuzi wake katika timu, mashabiki wa Simba wanatarajia kujionea mabadiliko fulani katika timu yao leo, ikicheza na timu dhaifu, Maji Maji.

Simba SC inaongoza Ligi Kuu kwa pointi zake 32, ikifuatiwa na Azam FC pointi 30 na Yanga SC pointi 28 ambazo zenyewe zimekamilisha mechi zake za duru la kwanza jana.
Azam FC jana ilishindwa kutumia vyema Uwanja wa nyumbani baada ya kuchapwa mabao 2-1 na Yanga SC Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

2 Comments

2 Comments

 1. Paul Kapele

  Paul Kapele

  January 28, 2018 at 11:08 am

  masoud djuma nakuomba sana ebu waelekeze wachezaji wote mfumo wako ule ule maana tayari walikua wameuzoea na mafanikio tulikua tunayaona.mi nina wasi wasi na huyo mfaransa yawezekana akabadili mfumo tena ikawa shida.tafadhari sana.

 2. Mohamed Zombôk

  Mohamed Zombôk

  January 30, 2018 at 5:48 am

  7

You must be logged in to post a comment Login

Leave a Reply

To Top