HTML Tables
Habari

MBUNGE WA CCM AHOJIWA KITUO CHA POLISI

MBUNGE wa Jimbo la Hangang kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Mary Nagu amehojiwa katika Kituo Kikuu cha Polisi kwa amri ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Sara Ali,  kwa kile kinachodaiwa kukaidi amri halali ya DC ya kuzuia mikutano ya mbunge huyo.

Inadaiwa Nagu na Mwenyekiti wa CCM Wilaya, Mathew Darema, waliwekwa ndani kwa saa kadhaa juzi kabla ya kuhojiwa.

Ikumbukwe kuwa, hii ni mara ya pili sasa kwa tukio kama hili kujitokeza kwa  Nagu wilayani humo ambapo Mara ya kwanza DC Sara aliwafikisha polisi Katibu wa CCM Wilaya na Mbunge wake kwa madai kuwa walifanya fujo katiika Kikao cha Kamati ya Siasa cha Wilaya

Click to comment

You must be logged in to post a comment Login

Leave a Reply

To Top