HTML Tables
Michezo

MBAO FC YAUNGANA NA SIMBA SC KWENYE FAINALI KOMBE LA FA

Kikosi Cha Mbao Fc

Klabu ya Mbao FC leo imeungana naklabu ya simba katika fainali ya kombe la Azam Sports Federation itakayochezwa mwezi mei 27 baada ya kuibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Yanga leo jioni.

Goli la dakika ya 27, lililotokana na krosi safi kutoka magharibi mwa uwanja uwanja na kuenda hadi kumbabatiza mchezaji wa Yanga Vicent Andrew Dante laipeleka klabu ya Mbao FC katika hatua ya fainali FA Cup.

Goli hilo ambalo limedumu hadi dakika 90  limesababisha wachezaji wa Yanga kukosa amani mnamo dakika za lala salama na kujikuta wakifanya kazi ya ziada ili kujaribu kurejesha goli hilo bila mafanikio,

Mchezo huo uliokua wa Nusu fainali ya wa kombe la Azam Sports Federation umejawa na vitimbwi vingu ambapo mda mchache kabla ya mchezo kuanza imeripotiwa kua moja ya wanachama wa klabu ya Yanga amejikuta aikipokea kipigo kutoka kwa mashabiki wa kandanda mjini Mwanza kwa madai ya kua alilazimisha kumwaga vitu uwanjani

Click to comment

You must be logged in to post a comment Login

Leave a Reply

To Top