HTML Tables
Habari

MAWAKILI UINGEREZA WAMTAKA RAIS MAGUFULI KUANZA UCHUNGUZI SUALA LA LISSU

Chama cha mawakili na watetezi wa haki za kibinaadamu nchini Uingereza wamemuandikia barua rais John Pombe Magufuli kikimtaka kuanzisha uchunguzi ulio huru mara moja kuhusu jaribio la mauaji lililotekelezwa dhidi ya mbunge wa Singida mashariki Tundu Lissu.

Wakili huyo ambaye pia ni rais wa chama cha mawakili nchini Tanzania TLS mnamo tarehe 7 mwezi Septemba alipigwa risasi tumboni na miguuni na watu wasiojulikana katika makaazi yake ya Dodoma.

”Ufyatulianaji huo wa risasi na maswala mengine ambaye yemetokeo yanayowahusisha mawakili yanatia wasiwasi”.

Ni muhimu mkubwa kwamba chama cha mawakili kinaheshimiwa kwa kuwa ni kitengo muhimu katika kuhakikisha kuwa sheria zinafuatwa kikamilifu, ilisema barua hiyo.

Barua hiyo ilisainiwa siku ya Jumatano na rais wa chama cha mawakili Joe Egan ,mwenyekiti wa baraza hilo Andrew Langdon na Mmwenyekiti wake Kirsty Brimelow.

Mawakili hao wamemwambia rais Magufuli pia kuanzisha uchunguzi kuhusu visa vyengine vya uhalifu vinavyotekelezwa dhidi ya mawakili.

Visa hivyo ni pamoja na mlipuko katika afisi ya mawakili ya IMMMA chini ya mwezi mmoja na tisho la waziri wa maswala ya kikatiba na sheria Harrison Mwakyembe la kutaka kufutilia mbali chama cha mawakili nchini Tanzania katika kipindi cha miezi saba iliopita.

5 Comments

5 Comments

 1. Nick Silas

  Nick Silas

  September 23, 2017 at 11:34 am

  Hapo sasa

 2. Japheth Simon

  Japheth Simon

  September 23, 2017 at 2:02 pm

  HAYO NDO MAMBO!

 3. Mpeka Jabir

  Mpeka Jabir

  September 23, 2017 at 3:54 pm

  Albadili imeanza kazi,hapo sasa

 4. Pingback: Maria Smith

 5. Pingback: Melanie Bowen

You must be logged in to post a comment Login

Leave a Reply

To Top