HTML Tables
Habari

MARUFUKU YA MICHANGO MASHULENI YAIBUA HISIA TOFAUTI

Kufuatia msimamo wa Raisi wa Tanzania John Pombe Magufuli kupiga maruku michango yote katika shule nchini Tanzania wadau wa sekta ya elimu wamekuwa na maoni mbali mbali

Michango hii imekuwa ikisaidia shughuli mbali mbali za maendeleo katika shule ikiwemo kusaidia upatikanaji wa chakula kwa wanafunzi sambamba na mahitaji mengine muhimu kwa shule hizo ikiwemo maji na ulizinzi

Meneja wa miradi ya haki elimu nchini Tanzania bwana Bonventure Geofrey amesema tamko hilo linashitusha kufuatia hali halisi ya shule nchini Tanzania kuwa zenye changamoto kubwa ikiwemo uchakavu na uhaba wa miundombinu kama vile madarasa , vyoo na maabara kwa shule za sekondari

Akizungumza baada ya tamko hilo waziri wa elimu sayansi teknolojia na mafunzo ya ufundi Joyce Ndalichako amewataka waalimu wote ambao tayari walikuwa wamekwisha kuchangisha fedha hizo kufanya utaratibu wa kurejesha kwa wazazi michango hiyo na kutoendelea tena na utaratibu huo ulipigwa marufuku

Serikali ya wamu ya tano nchini Tanzania ilitangaza kutoa elimu bure katika ngazi ya elimu msingi ambayo ni kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne.

Rais wa Tanzania amesema kwamba walimu watakaopatikana wakiwalipisha fedha wazazi ili kulipia elimu ya wanao watafutwa kazi.

Serikali ilianzisha elimu ya bila malipo katika shule za majimbo yote nchini humo mwaka 2015 .

Lakini rais Magufuli amesema kuwa baadhi ya shule zinaendelea kulipisha karo na malipo mengine ya chakula, ziara za masomo na huduma nyenginezo.

Wanafunzi wasiolipa fedha hizo hulazimika kurudi nyumbani .

Click to comment

You must be logged in to post a comment Login

Leave a Reply

To Top