HTML Tables
Burudani

MANENO YA EMMANUEL MBASHA BAADA YA NDOA YA FROLA

Muimbaji  wa nyimbo za Injili nchini Tanzania, Emmanuel Mbasha ambaye alikuwa mume wa Mwanamama Flora Henry amefunguka na kuweka wazi kwa kila kitu kuwa Mrembo huyo ni mtu wa kuruka kuruka kwa Wanaume kwani anaendeshwa na tamaa.

Mbasha amesema Flora amezoea maisha ya kurukaruka na wanaume kwani hata yeye licha ya kumtoa kijijini na kumleta mjini bado alimkimbia kwa tamaa ndogo ndogo.

“Unajua Flora amechaguwa kuwa na maisha ya kurukaruka, kwani hata baada ya mimi alikuwa na wanaume wengine kadhaa, saizi kaolewa  tena akiona maisha magumu huko aliko atakwenda kwa mwingine hayo ndiyo maisha aliyochagua.“Alisema Emannuel Mbasha na kusisitiza kuwa, Flora hakumuacha kwa sababu ya Kuporomoka kiuchumi.

“Mimi nilikuwa na pesa muda mrefu ndiyo maana nilimchukua  Flora na kumleta mjini, tukaanza maisha pamoja, nikamuuingiza studio akaanza kurekodi na Watanzania kumjua, hivyo pesa nilikuwa nazo maana ningekuwa sina pesa sidhani kama angekubali kuolewa na mimi,“Alisema Emannuel Mbasha kwenye Mahojiano yake na EATV.

Flora Henry aliachana na Emannuel Mbasha kwa mvutano kwenye ndoa yao ambayo ilibarikiwa kupata mtoto mmoja wa kike na tayari mrembo huyo ameshafunga ndoa nyingine ya pili wikiendi iliyopita na Mwanaume mwingine huko Jijini Mwanza

1 Comment

1 Comment

  1. Patrick Kasonso

    Patrick Kasonso

    May 3, 2017 at 12:15 pm

    Shetani kamloga, kasahau alikotoka kwa tamaa za dunia! hata huyo hatadumu naye kwani amemkufuru mungu kufunga ndoa marambili, akiachana na huyo atampata mwingine atafunga ndoa ya tatu! aibu kweli kweli..

You must be logged in to post a comment Login

Leave a Reply

To Top