HTML Tables
Michezo

LEICESTER CITY YASHINDA 2-0 KOMBE LA FA

Nyota Mnigeria, Kelechi Iheanacho (kulia) akishangilia baada ya kuifungia mabao yote mawili Leicester City dakika za 43 na 77 ikishinda 2-0 dhidi ya Fleetwood ya Daraja la Kwanza katika mchezo wa Kombe la FA jana Uwanja wa King Power, Leicester.

Hata hivyo, kwa bao la pili ilibidi kwanza refa Jon Moss athibitishiwe kupitia teknolojia ya picha za video (VAR) kwamba Iheanacho hakuwa ameotea baada ya awali kukataliwa akidhaniwa alikuwa ameotea. Iheanacho anaweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza England bao lake kuhalalishwa na mfumo wa VAR baada ya awali kukataliwa kwa kudhaniwa ameotea

Click to comment

You must be logged in to post a comment Login

Leave a Reply

To Top