HTML Tables
Burudani

KWA NINI BASATA WALIMTENGA RAYVANNY?

RAYVANNY.

MAPYA YA BASATA NA RAYVANNY..!

Siku mbili baada ya mwimbaji Rayvanny kuwasili Bongo na kukutana na mapokezi makubwa Airport DSM akiwa na tuzo yake ya BET akiwa msanii kwanza wa Bongofleva kutwaa tuzo hiyo, sgumzo ni kuhusu kutooneakana mwakilishi wa BASATA Airport.

255 ya XXL ya Clouds FM jana June 29, 2017 imempata Katibu Mkuu wa BASATA, Godfrey Mngereza ambaye ameelezea sababu za kutoonekana mwakilishi wa Baraza hilo akisema kulikuwa na mawasiliano finyu kati ya Rayvanny na BASATA wakati anakwenda na kurudi kuchukua tuzo hiyo.

“Hakukuwa na mawasiliano mazuri alivyokuwa amekwenda na ujio wake lakini tungekuwa tunaifahamu ratiba yake Baraza kama ilivyo ada huwa hatuna budi ya kwenda kumpokea Airport, kwanza inaleta heshima. 

Kwa hiyo, hakuna sababu ya kusema tusingeenda kumpokea ni kwamba

mawasiliano hayakuwepo tangu anaenda na pia ningependa nikumbushe wasanii wanavyokwenda nje ya mipaka ya Tanzania ni vizuri tukaagana ili tukajua ratiba ikoje hata wakirudi tuwapokee”. Mngereza.

Click to comment

You must be logged in to post a comment Login

Leave a Reply

To Top