HTML Tables
Burudani

KUTOKA FLORA MBASHA MPAKA FROLA KUSEKWA

Na Thomas Samson

Mwanadada mahiri katika tasnia ya muziki wa injili “Madam flora” amefunga ndoa jana 30 April 2017 na aliyekuwa mchumba wake David kusekwa.Ndoa hiyo imemfanya kupata jina la flora kusekwa ikiwa ni mwaka mmoja tu tangu kuachana na aliyekuwa mumewe Emmanuel Mbasha.

Ndoa hyo iliyofungwa jijini Mwanza ilisindikizwa na uzinduzi wa albamu ya wawili hao na hivi sasa tayari wamekwishaingia mapumzkoni(honeymoon)

“Siku zote nilikuwa natamani mwanaume atakaye nijali na kuniheshimu” ni maneno aliyowahi kutamka Flora kabla ya kutangazwa kwa uchumba wake na David kusekwa.

Hata hivyo asilimia kubwa  ya mashabiki wa Flora wameonesha kutofurahishwa na kitendo cha mwanadada huyo kufunga ndoa mapema Kiasi hicho,wengine wakiamini si vizuri ki maadili ya dini ya kikristo.

Click to comment

You must be logged in to post a comment Login

Leave a Reply

To Top