HTML Tables
Michezo

KOCHA SINGIDA AIKUBALI KAZI YA SIMBA SC JANA TAIFA

Kocha Mkuu wa Singida United, Mholanzi, Hans van der Pluijm, amesema kuwa licha ya kupoteza mchezo wa jana dhidi ya Simba, lakani sifa nyingi ni kwa timu yake kutokana na kujituma lakini bahati haikuwa upande wao.
Singida ilikubali kichapo cha mabao 4-0 dhidi ya Simba, kwenye mchezo wa raundi ya 13 ya Ligi Kuu Bara, uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Akizungumza baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Pluijm alisema kuwa, anawapongeza sana Simba kwa ushindi huo mnono na kilichotokea ni matokeo ya mchezo hvyo atakwenda kufanya marekebisho ya makosa yao.
“Unaweza kuona ni jinsi gani sina furaha leo, kilichotokea ni moja ya mchezo, vijana wangu walikuwa vizuri lakini bahati leo haikuwa yetu, tunahitaji kufanya kazi kubwa kurekebisha makosa,” alisema Pluijm.

Click to comment

You must be logged in to post a comment Login

Leave a Reply

To Top