HTML Tables
Michezo

KOCHA HUYU APONDA KIWANGO CHA SIMBA SC

Baada ya kuilazimisha Simba sare ya mabao 3-3 katika mchezo wa Ligi Kuu Bara Ijumaa ya jana, Kocha Msaidizi wa Stand United, Athuman Bila Bilo, amezidi kusema Simba ni ya kawaida.

Akizungumza na Saleh Jembe asubuhi ya leo, Bilo amesema katika mpira siku zote hakuna kudharau timu kwa maana kila upande unakuwa una maandalizi yake ya kupata alama 3, japo halikufanikiwa hilo.

“Unajua katika mpira huwa kuna matokeo matatu, kwa namna tulivyokuwa tumejipanga hayo matokeo tuliyoyapata tunashukuru, Simba ni timu ya kawaida, tushaisahau na sasa akili zetu tunazihamishia kwenye mchezo ujao dhidi ya Tanzania Prisons” amesema Bilo.

Katika mchezo wa jana, Simba ilikuwa inaruhusu mabao zaidi ya mawili tangu msimu huu wa ligi uanze, huku Aishi Manula akifungwa goli la kwanza la moja kwa moja kwa njia ya kona tangu ajiunge na Simba.

Click to comment

You must be logged in to post a comment Login

Leave a Reply

To Top