HTML Tables
Michezo

KILICHOIPONZA YANGA SC HUKO BOTSWANA CHATAJWA

Nahodha wa klabu ya Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, ameweka wazi sababu iliyowafanya washindwe kusonga mbele kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

Yanga ilishindwa kufuzu baada ya kupoteza kwa jumla ya mabao 2-1 dhidi ya Township Rollers ya Botswana, kwa ‘Aggregate’ na kuaga rasmi uwepo wao kwenye mashindano.

Akizungumza baada ya mchezo, Cannavaro alisema sababu kubwa iliyowafanya washindwe kusonga mbele ni kushindwa kutumia faida ya Uwanja wa nyumbani.

“Kikubwa mabacho kimesababisha tusiweze kusonga mbele ni kushindwa kutumia Uwanja wa nyumbani, mashindano haya unapocheza ugenini kunakuwa na mambo mengi, jambo ambalo limetugharimu” alisema.

Licha ya kuondolewa kwenye mashindano hayo, Cannavaro amesema nguvu zao zote hivi sasa wanazihamisha katika Kombe la Shirikisho Afrika walipokuwa wanashiriki Simba.

Click to comment

You must be logged in to post a comment Login

Leave a Reply

To Top