HTML Tables
Elimu

JE WAJUA? HAYA NI MAMBO 10 YA KUKUMBUKA KUHUSU BABA WA TAIFA MWALIMU NYERERE

Baba wa Taifa la Tanzania, Mwl Julius Kambarage Nyerere.

MAMBO KUMI (10) YA KUJUA KUHUSU MWALIMU NYERERE.

1. Baba yake alikuwa ni Chifu na alikuwa na wake 22.

 

2. Mwalimu alibahatika kusoma kwa bahati tuu!. Ndugu wengine wote kwa Baba, ukiachia wa tumbo la Mama yake, waliishia kuchunga mbuzi!.

 

3. Baba Yake Mwalimu, alikataa Ukristo kata kata!. Wamishenari walipomshawishi kuachana na dini asili na kujiunga na Ukristo, aliwauliza Ukristo una nini ambacho dini za asili hazina!. Walimjibu, Upendo, Amani, Unyenyekevu, Utii, Haki etc, aliwajibu tena kwa mifano hai jinsi nazo dini za asili zinavyohubiri Upendo, Amani, Unyenyekevu, Utii na Haki.

 

4. Alianza shule akiwa na miaka 12, na darasani alikuwa na akili sana hivyo akarushwa baadhi ya madarasa!.

 

5. Akiwa Tabora School ndipo alipo pokea Ukristo kwa kubatizwa jina la Julius ambalo alilicopy toka kwa Julius Ceaser!

 

6. Akiwa Tabora School, alikuwa ni mtoto mkaidi sana!. Adui zake wakuu walikuwa ni viranja!. Alishitakiwa mara kadhaa kwa mwalimu mkuu na ukafikia wakati Mwalimu Mkuu akaamua Julius afukuzwe shule!. Mwalimu wake wa darasa licha ya utundu wake, alimpenda sana kwa sababu alikuwa na akili sana!. Hivyo akamnusuru kufukuzwa shule kwa kumfanya na yeye awe kiranja.

 

7. Kwa mujibu wa maneno ya Mzee Dossa Aziz anamwelezea Nyerere kuwa, wakati wa kudai uhuru siku za mwanzo TANU ilikuwa haina usafiri ukiacha baiskeli mbovu iliyokuwa ikitumika pale TANU Headquarters New Street. 

Dossa akawa na kawaida ya kumpenyezea Nyerere kibahasha chenye fedha ili kimsaidie katika shughuli za siku kama usafiri na mahitaji mengine.

 

Dossa anaendelea kusema kuwa kila ikifika jioni wakikutana Nyerere alikuwa akimrudishia ile bahasha hata senti moja Nyerere hakutumia au kama imemlazimu atumie kiasi cha fedha basi fedha zilizobaki ikiwa palikuwa na matumizi lazima atazirudisha. 

 

Dossa akimuuliza Nyerere imekuwaje mbona umerudisha? basi Nyerere atamwambia,

”Dossa basi hata safari ya Ilala nichukue taxi? Nimepanda DMT.”

 

Hii DMT kirefu chake ni Dar es Salaam Motor Transport ndiyo walikuwa wakitoa huduma ya public transport Dar es Salaam.

 

8. Alitakiwa kuozeshwa mwanamke awali kabla ya Mama Maria, lakini mpango haukukamilika.

 

9. Alipata matatizo sana ya kifedha alipoenda kusoma Uingereza mpaka kuna kipindi aliiandikia serikali ya kikoloni imfadhili na akataka kukatisha masomo yake kurudi Tanzania.

 

10. Alipendwa sana na kaka yake, marehemu Chifu Edward Wanzagi. Edward Wanzagi ndiye aliyemshawishi baba yao Chifu Burito Nyerere amsomeshe Kambarage, baada ya kumuona Kambarage alivyokuwa anawachachafya watu wazima katika mchezo wa bao akiwa na umri mdogo hivyo kaka yake huyo akagundua kuwa Mwalimu alikuwa na akili zisizo kawaida.

1 Comment

1 Comment

  1. Pingback: Maria Smith

You must be logged in to post a comment Login

Leave a Reply

To Top