HTML Tables
Habari

HUYU NDIYE MSHINDI WA 28 ALIYEJISHINDIA TVS KING SPORTPESA

Hatibu Mganga Mohamed (39) dereva kivuko Kigamboni alipokea habari za furaha alipopigiwa simu na timu ya SportPesa na kufahamishwa kuwa yeye ndiye mshindi wa 28 wa pikipiki ya matairi matatu aina ya TVS KING DELUXE kutoka promosheni ya SHINDA NA SPORTPESA.
Mshindi huyo alijawa na furaha kwani kipindi alichokuwa akipokea taarifa hizo alikuwa anapitia kipindi kigumu kidogo. Wakati akikabidhiwa zawadi yake, mshindi huyo aliipeleka timu ya SportPesa nyumbani kwake ambapo ni chumba kimoja kilichopigwa alama ya X nyekundu ikimaanisha inatakiwa kuvunjwa kwa madhumuni ya kupanua barabara.
Mshindi alisikika akisema, ameanza kuweka ubashiri na SportPesa ndani ya mwezi mmoja na alipopewa taarifa ya ushindi amepata matumaini kwani ingawa anatarajia kupoteza makazi yake, lakini kipato atakachopata kupitia biashara ya bajaji kitamsaidia kutunza familia yake na kulipia ada za shule za watoto wake wawili ambao wanasoma shule binafsi.

Mkazi huyo wa Ubungo Kibo alikuwa na ndugu, jamaa na marafiki ambao walifurahia ushindi wake na kuhamasika pia kuweka ubashiri na SportPesa kwani Promosheni hiyo ni ya kweli na Watanzania wote wana nafasi ya kujishindia TVS KING DELUXE kama yeye alivyoshinda.

Click to comment

You must be logged in to post a comment Login

Leave a Reply

To Top