HTML Tables
Michezo

HUU NDIO MTAMBO MPYA WA MABAO ARSENAL

Haya ni baadhi ya mambo ambayo huenda huyajui kuhusu Pierre-Emerick Aubameyang, katika maisha mtoto hufuata matarajio ya wazazi na wazazi husaidia kwa kila hali kufanikisha ndoto za mtoto huyo, Pierre-Emerick aliwahi kumuahidi babu yake kuwa siku moja ataichezea Real Madrid, hayo ni maneno machache aliyozungumza Aubameyang na babu yake kabla babu yake hajafariki.

Mama yake aubameyang alifichua Disemba mwaka jana kuwa ndoto ya mwanae ni kuichezea Madrid siku moja na familia nzima ipo nyuma ya hilo, kwa Aubameyang kwenda Arsenal anaweza kuwa amefuta ndoto ya familia kumuona kwenye jezi ya Real Madrid.

Aubameyang yupo karibu na baba yake na ndiye aliyemshauri acheze Borussia Dortmund kuliko kuichezea timu ya ligi daraja la kwanza, Pierre anafuata nyayo za baba yake ambaye pia aliwahi kuwa nahodha wa timu ya taifa ya Gabon akicheza kama mlinzi, alifanikiwa kucheza michezo 80 kabla ya kuajiriwa kuwa msaka vipaji wa klabu ya AC Milan.

Aubameyang ambaye ni nyota wa zamani wa Dijon ambaye kwa sasa ni mfungaji wa muda wote wa timu ya taifa ya Gabon na nahodha wa timu ya taifa hilo aliwahi kupewa nafasi ya kuichezea timu ya taifa ya Italia kutokana na Aubameyang kukaa kwa muda mrefu italia hivyo ikawa rahisi kuaminiwa kuichezea timu ya taifa ya Italia maarufu kama Azzurri.

Alianza kukataa kuichezea timu ya taifa ya Italia chini ya 19 kabla ya kukataa kuichezea Azzurri, Aubameyang alizaliwa Ufaransa alikuwa na uwezo wa kuichezea timu ya taifa kama ilivyokuwa kwa Italia, ingawa KWA Ufarasa alikubali kuichezea timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 21.

Baada ya kutwaa ubingwa wa ligi ya mabingwa barani Ulaya FC Porto, Jose Mourinho alijiunga na Chelsea alijitangaza kuwa yeye ni ‘Special One’ kwenye mkutano wa kwanza na waandishi wa habari nchini England. Aubameyang anaweza kumuiga Mourinho kwa kujitangaza kuwa First One akichagizwa na historia na rekodi zake alizowahi kufikia, ya kwanza ile ya kuwa mgabon wa kwanza kucheza Ujerumani pia alifunga hat-trick yake ya kwanza alipoichezea kwa mara ya kwanza Borussia Dortmund kwenye ligi.

Anaweza kufanya hivyo England na ikawa rahisi kwa watu kumtamka kama first one, Aubameyang pia ni mgabon pekee kufunga goli kwenye michuano ya Olympic alipokwamisha mpira wavuni dhidi ya Switzerland kwenye hatua ya makundi mwaka 2012, hiyo moja ya sifa inayomfanya aitwe first one.

Huu ni kweli ambao unawaumiza wakazi wa jiji la Milan na mashabiki wa timu hiyo, pamoja na Aubameyang kuzaliwa Ufaransa baba yake alihamia Italia na kupata kazi ya kuwa mtafutaji vipaji wa AC Milan baba yake alimpendekeza mtoto wake aingie kwnye academy ya San Siro maafisa wa Milan hawakuamini kwenye uwezo wa Aubameyang hivyo basi, baba yake akampeleka mwanae kwenye klabu ya Saint Etienne ni huko Ufaransa ambako nyota yake iling’ara mpaka akaonwa na Borussia Dortmund.

Kaka zake nao walipita kwenye academy ya Milan kabla ya kutimkia kwingine waza tu Milan ingekuwa na mmojawao kipindi hiki ambacho wana uhaba wa magoli, uharaka na mbio ni vitu vinavyowatofautisha wachezaji wengi duniani, wakati Gareth Bale alipomuaibisha Marc Batra kwenye fainali ya kombe la Copa del Rey mwaka 2014, Madridistas walifurahishwa sana na kitendo hicho, kitu kama hicho ndio kinawafurahisha mashabiki wa Dortmund kila wiki kwenda viwanjani kumuangalia Pierre-Emerick unaweza unaweza kuhisi ni chui anakimbiza mtu au mnyama huwapita walinzi kwenye hali mbaya wakipoteza muda kwenye kukaba kivuli, speed meter ilibainisha mshambuliaji huyo wa Dortmund anakimbia mita 30 kwa sekunde 3.7 kitu kilichomvutia hata mkimbiaji Usain Bolt.

Click to comment

You must be logged in to post a comment Login

Leave a Reply

To Top