HTML Tables
Michezo

HIVI NDIVYO SIMBA SC ILIVYOPEWA SOMO NA MWANASAIKOLOJIA

Daktari na Mtaalamu wa masuala ya Saikolojia, Chris Mauki, ametoa somo kwa wachezaji wa Simba katika Hotel ya Sea Scape iliyopo jijini Dar es Salaam.

Mauki ametoa somo la namna ya mchezaji anapaswa kujijengea ujasili pale anapokuwa ndani ya uwanja.

Mtaalamu huyo ameeleza namna mchezaji anapaswa kujitambua na kujiamini pindi anapokuwa uwanjani wakati wa mechi ili kuisaidia timu kupata matokeo chanya.

Somo hilo kwa wachezaji wa Simba limekuja kufuatia maandalizi ya mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya A Masry SC utakaopigwa Jumatano ya wiki hii Uwanja wa Taifa.

Click to comment

You must be logged in to post a comment Login

Leave a Reply

To Top