HTML Tables
Habari

HISA ZA SIMBA ZAAMSHA DUDE, BAKHRESSA NA MO DEWJI WAWASHA MOTO

BHAKRESA AMPA CHALLENGE MO SIMBA SC

 

Juzi Simba walitangaza kuanza kuuza hisa za klabu hiyo ambayo walisema mtu ambaye anataka kuinunua simba kwa asilimia 50 lazima aweke dau la shilingi kuanzia bilioni 20 na kuendelea. Kamati ya Dokta Mihayo imetangaza hivyo ila kwa masharti anayetaka kununua hisa za klabu lazima awe mwanachama wa klabu hiyo na masharti mengine

 

Wanachama wengi wa Simba walijua Mohamed Mo tajiri kijana Afrika nzima ndio mwenye uhakika wa kununua hisa asilimia 50 kwani yeye alionesha nia tangu mwanzo na kujitahidi kuisaidia simba kwa namna moja au nyingine. Watu wengi walijua hivyo hata mimi nilijua kabasa simba ni ya Mo na Mo ni wa simba .

 

Habari za kuaminika kutoka ndani ya Simba zinasema tajiri Said Salim Bhakresa ameweka mpunga mrefu zaidi wa bilioni 25 kutaka kununua hisa asilimia 50 ndani ya klabu ya simba na Bhakresa ametimiza kigezo cha mwanachama kwani yeye ni mwanachama wa Simba na ana kadi ya Simba sc.

 

Baada ya kutokea habari ya Bakhresa kutaka kununua hisa asilimia 50 ndani ya Simba hali imekuwa si hali viongozi Simba wanamtaka Mo Dewji wengine wamemuomba aongeze dau liwe zaidi ya billion 25 ili wampe timu ilhali wengine wakisema atoe hiyo 20 tu kwani Mo ameisaidia sana simba na ametoa Bilioni moja kwenye bilioni 20 ili kusaidia uendeshaji wa Timu. Na wakaenda mbali wakasema mwanachama  bhakresa alikuwa wapi kuisaidia klabu mwanzo.

 

Kamati ya Dokta Mihayo inaendelea na mchakato huo ili kupata mtu sahihi ambaye atawekeza. Baada ya kutafutwa mihayo kuzungumzia suala la Bakhresa kutoa dau la bilioni 25 alisita kuweka wazi zaidi ya kusema mchakato unaendelea na ukifikia mwisho tutatoa statement ya kamati wangapi wameonyesha nia na wangap wamekidhi vigezo vya kuchaguliwa kuwa wawekezaji ndani ya Simba SC.

4 Comments

4 Comments

 1. John Gabriely

  John Gabriely

  October 12, 2017 at 3:20 pm

  Duuuh nihatari sana mafahar wawili wakutaba sasa hapo ni mwenyekisu kikari ndo atakula nyama

 2. Joseph Mukono

  Joseph Mukono

  October 12, 2017 at 5:28 pm

  Mo aonyeshe kweli kama yeye ni tajiri number moja wa uhakika,manake Said Salim Bakhresa & Co, cjui kwanini na vitu gani anazidiwa na Mo. ok,nisiseme sana manake mimi sio mchumi,mimi ni Fundi tu.

 3. Osward Mwambete

  Osward Mwambete

  October 13, 2017 at 9:19 am

  Duu! Hii Vita ngumu sana.Lakini Kwa sababu Anaeshinda ni mmoja BASI tusubilie ninani atashinda kati ya hawa Wawili

 4. Faadhil Hadji

  Faadhil Hadji

  October 13, 2017 at 3:35 pm

  Hivi na bakhresa naye ni mwanachama wa mnyama au figisu tu!!

You must be logged in to post a comment Login

Leave a Reply

To Top