HTML Tables
Michezo

HAYA NDIO MAENDELEO YA OKWI BAADA YA KUUMIA JANA

Mshambuliaji Emmanuel Okwi alipigwa kwenye koo baada ya kupigwa ngumi.
Hali hiyo ilisababisha ashindwe kupumua na kulazimisha mwalimu wake Kocha Pierre Lechantre kulazimika kumpumzisha.
Okwi alipigwa ngumi na beki wa Ruvu Shooting ambaye alitolewa kwa kadi nyekundu.
Msemaji wa Simba, Haji Manara amesema mchezaji huyo anaendelea vizuri ingawa alishindwa kupumua baada ya tukio hilo.

“Alipata maumivu baada ya kupigwa ngumi, unajua ngumi ya kisukusuku kwenye koromeo si jambo dogo.
“Lakini tunashukuru anaendelea vizuri na tunatarajia tutakuwa naye kambini maandalizi dhidi ya Azam,” alisema.
Okwi alitolewa baada ya kupigwa kwa makusudi na beki huyo na Ruvu Shooting walicheza kindava wakionekana walikuwa wamepania kuwaumiza wachezaji wa Simba kama ambavyo walicheza kindava katika mechi dhidi ya Yanga ambayo walilala kwa bao 1-0 lakini mshambuliaji Yohana Nkomola naye alitolewa baada ya kuumizwa na hadi sasa ni majeruhi.

Click to comment

You must be logged in to post a comment Login

Leave a Reply

To Top