HTML Tables
Michezo

HATIMAYE SIMON MSUVA KUONDOKA TANZANIA JUMATANO WIKI HII

Winga wa Yanga SC, Simon Msuva anatarajiwa kuondoka nchini Jumatano kwenda Morocco kwa ajiloi ya kukamilisha uhamisho wake kujiunga na Difaa Hassani El-Jadida ya Ligi Kuu ya nchini humo.

 

Difaa ambayo tayari imekwisha mchukua Mtanzania mwingine, winga pia Ramadhani Singano ‘Messi’ kutoka Azam FC iko tayari kutoa dola 150,000 kumnunua Msuva ambaye amebakiza miezi tisa katika mkataba wake Yanga.

 

Msuva amesema kwamba akifuzu vipimo vya afya atasaini moja kwa moja mkataba wa kujiunga na timu hiyo ya Ligi Kuu ya Morroco.

Msuva amerejea Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo kutoka mjini Kigali alipokuwa na kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania kwa ajili ya mchezo na wenyeji, Rwanda kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN.

5 Comments

5 Comments

  1. Pingback: ABrand

  2. Pingback: free bitcoin cash

  3. Pingback: nileriver

  4. Pingback: cupooftea

  5. Pingback: Top 10 Best

You must be logged in to post a comment Login

Leave a Reply

To Top