HTML Tables
Burudani

HARMO RAPA: NGOMA YANGU MPYA NI SHEEDA!

Msanii anaechipukia kwenye game ya muziki wa Hip Hop ‘Harmorapa’ ametoa onyo kali kwa wasanii wa muziki barani Afrika kwa ujio wa ngoma yake mpya anayotarajia kuiachia, ambayo ameahidi itakuwa ni ‘Bomu’ litakalowasambaratisha wasanii. Hamorapa amewataka wasanii watumie muda huu kuachia ngoma zao.

Harmorapa amesema ngoma yake mpya itafunika wasanii wote wakubwa barani Afrika huku akisisitiza kuwa ni vyema wakaachia ngoma zao kwa muda huu, kwani wakichelewa huenda wakapatwa na Bomu hilo ambalo litawafanya wasisikike kabisa kwenye ramani ya muziki.

“Mashabiki wangu nawaletea Bomu litakalo sambalatisha ngoma za wasanii wote Africa naposema Bomu simaanishi kabomu ka mkono ka mh #trump hapana namaanisha Bomu LA nyuklia la kiduku linalo milikiwa na kolea kusin so nawakanya na wasanii wote Africa walioficha vinyimbo vyao ndani wavitoe haraka sasa hivi kabla Mimi sijaachia Bomu langu kwani nikiachia hamto sikika tena”,Ameandika Harmorapa kwenye ukurasa wake wa Instagram

Click to comment

You must be logged in to post a comment Login

Leave a Reply

To Top